Takribani eneo zima la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo limetapakaa madini aina mbali mbali, inasemekana zipo aina 25 za madini zimegundulika ambazo baadhi yake utafiti wa kina unafanyika ili kupata kiwango cha uwepo wake.
Uchimbaji wa madini yaliyopo si wa kitaalamu yaani wa kutumia nyenzo za kisasa kuweza kuzalisha kiasi kikubwa cmadini ukilinganisha na uwezo wake.Aina za madini yapatikanayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ni Dhahabu, Shaba, Fedha, Risasi, Tungsten, Rose Quarts na Nitre.
Madini ya Dhahabu yanachimbwa katika maeneo ya Machimboni, Uruwira, Kapapa, Singililwa, Society, Katisunga, Ibindi, Itenka, Sitalike. Madini ya Shaba yanapatikana katika maeneo ya Ibindi, Ugalla, na Singililwa.
Madini ya fedha hupatikana kwenye maeneo ya Ibindi, Sikitiko na Kapalala. Pia, madini ya Risasi hupatikana Nsimbo na Uruwira. Madini ya Tungsten hupatika Ibindi Njiapanda, wakati madini ya Rose Quarts na Nitrate hupatikana huko Ugalla.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa