Friday 9th, May 2025
@ARUSHA
Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 8 Machi, 2025 kitafanyika Kitaifa Mkoani Arusha na kutatanguliwa na maadhimisho katika ngazi ya Mikoa nchi nzima ili kuwa na ushiriki wa Wanawake na jamii kwa wingi zaidi. Siku ya kilele, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
kaulimbiu ya mwaka huu ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” ambayo imetokana na Kaulimbiu ya Kimataifa ‘’For All Women and Girls. Equality. Rights. Empowerment’’. Lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kukuza Usawa, Haki na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana na kwa kuzingatia kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ili, wajiamini, wajiandae na wajitokeze kugombea nafasi za uongozi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa