Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuph Kimaro, amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, kushiriki kikamilifu katika shughuli za utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha jamii inabaki na mazingira safi na salama kwa ustawi wa afya na maendeleo ya Taifa.
Akizungumza Novemba 26, 2025 katika shule ya Sekondari Nsimbo wakati wa kampeni ya uhamasishaji na utunzaji wa mazingira inayoandaliwa na Shirika la Habari la Taifa (TBC), Mhe. Jamila, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi, amesema kuwa ushiriki wa wananchi ni nguzo muhimu katika kulinda mazingira.
Amesisitiza umuhimu wa mkoa kuungana na Mwanamazingira Namba Moja, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika juhudi za kukijanisha nchi.
“Leo ni fursa kwa wana Katavi kuungana na Mwanamazingira Nambari Moja, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kukijanisha mkoa wetu. Tayari tumepanda zaidi ya miti 300 kando ya barabara ya Mpanda–Tabora na katika shule ya Sekondari Nsimbo ili kuboresha mazingira,” alisema Mhe. Jamila.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuendelea kulinda amani kwa kuepuka kushiriki katika matukio au viashiria vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa nchi, na badala yake kuelekeza nguvu katika shughuli za uzalishaji mali na uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu.
Kampeni ya Mti wa Mama 27 ya Kijani, inayoratibiwa na TBC, inalenga kuhamasisha jamii kutunza na kuboresha mazingira ili kuwa na mazingira safi, salama na rafiki kwa shughuli za kibinadamu.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa