Saturday 18th, October 2025
@HOSPITALI YA WILAYA YA NSIMBO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nsimbo Bi. Christina Daniel Bunini anawakaribisha Wananchi wote wa Nsimbo katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo kwa ajili uchunguzi wa afya zao na kupata huduma za matibabu ya magonjwa mbalimbali.
Zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku 5, kuanzia Septemba 29, 2025 hadi Oktoba 3, 2025 katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo.
Katika zoezi hilo kutakuwa na Timu ya Madaktari saba (7) wabobevu;
(1) Daktari bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Ukunga
(2) Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto na watoto Wachanga
(3) Daktari bingwa wa Upasuaji
(4) Daktari bingwa wa usingizi
(5) Daktari bingwa wa Magonjwa ya ndani
(6) Daktari bingwa wa Magonjwa ya kinywa na meno
(7) Mkunga mbobezi
Gharama za huduma katika zoezi hili zitakuwa nafuu, na vilevile Kadi za bima za NHIF zitatumika kwa wale watakaokuwa nazo. Wananchi wote wa Wilaya ya Nsimbo wanasisitizwa kuitumia vyema fursa hii.
Aidha zoezi hilo pia linatarajiwa kuendeshwa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi ikiwemo Mpanda Manispaa, Mlele, Mpimbwe na Tanganyika.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa