Na: John Mganga-IO Nsimbo DC
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeidhinishiwa kupokea kiasi cha Shilingi 2,550,000,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo fedha hizo zimeelekezwa kwenye maeneo ya vipaumbele vinavyogusa Wananchi moja kwa moja kwa ajili ya kuwaondolea kero katika kuzifikia huduma za Elimu na Afya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Halawa Charles Malendeja pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada mbalimbali anazofanya katika kufufua uchumi kwa sekta zilizopata athari za kiuchumi kutokana na madhara ya UVIKO 19.
Katika Taarifa yake mbele ya kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kilichoketi 21 Oktoba 2021,Mkuu wa Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji Nsimbo Viktoria Cilewa ameeleza kuwa kati ya fedha hizo zilizotolewa,Shilingi 860,000,000.00 zitatumika kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba 43 vya madarasa kwa ajili ya kujiandaa kupokea Wanafunzi wa kidato cha kwanza watakaojiunga Mwezi Januari 2022 ambapo ujenzi huo utajumuisha pia utengenezaji wa viti na meza 2150 na kwamba Idadi ya vyumba vya madarasa utatofautiana kutoka shule moja hadi nyingine kulingana na mahitaji.
Amezitaja Shule za Sekondari Nsimbo zitakazonufaika na Fedha hizo kuwa ni Shule ya Sekondari ya Itenka,Ivungwe,Kanoge,Katumba,Kenswa,Kaboronge,Mtapenda,Nsimbo,Sitalike,Ugalla River,Uruwira pamoja na Shule ya Sekondari ya Machimboni ambazo kila moja itapokea fedha hizo kulingana na mahitaji yaliyopo.
Kwa upande wa Elimu msingi kiasi cha Shilingi 880,000,000.00 kimeelekezwa kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba 44 vya madarasa katika vituo shikizi 11 ambavyo hutumika kwa ajili ya kufundishia Wanafunzi wa Awali hadi darasa la tatu wanaokaa mbali na Shule mama ambapo imeelezwa kuwa hatua hiyo, itapunguza adha ya umbali kwa Wanafunzi 1980 na hivyo kupunguza kuondoa kabisa tatizo la utoro ambapo pia ameeleza kuwa ujenzi huo utaendana na utengenezaji wa madawati 660 ambapo kila chumba kitakuwa na madawati 15.
Amevitaja vituo shikizi vitakavyonuifaika na fedha hizo kuwa ni Motomoto,Kalele,Kamini,Kazaroho,Sikwisi,Mtambo B,Tulieni,Imilamate,Jilabela,na kituo Shikizi cha Magula ambapo kila kimoja kitapatiwa kiasi cha Shilingi Mil.20
Akizungumzia kuhusu Sekta ya Afya Afisa Mipango Nsimbo ameeleza kuwa Kiasi cha Shilingi Milioni 810,000,000.00 zimeelekezwa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Afya Nsimbo ambapo kati ya hizo Shilingi 300,000,000.00 zitatumika kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la huduma ya dharura(EMD) katika Hospitali ya Halmashauri .Aidha Shilingi Milioni 420,000,000.00 zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa Jengo la X-RAY,pamoja na Shilingi Mil 90,000,000.00 zilizobaki zimeelekezwa kwenye Ujenzi wa Nyumba vya Watumishi kwa vituo vilivyoko mbali na Makao makuu.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa