Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi kwa mara ya kwanza imefanikiwa kutoa huduma ya upasuaji kwa wanawake waliofika Hospitalini hapo kwa lengo la kupata huduma ya uzazi.
Kupitia uboreshaji wa miundombinu iliyofanyika katika sekta ya afya, Hospitali hiyo imefanikiwa kutoa huduma ya upasuaji kwa wanawake wawili waliofika kupata huduma ya uzazi tarehe 12 February 2026 baada ya kupewa rufaa kutoka kituo cha afya Katumba.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo Dkt. Patrick Tulyanje amesema Madaktari na wauguzi walifanikiwa kuwapatia huduma ya dharua ya kuijifungua kwa njia ya upasuaji wajawazito wawili waliofika kupata huduma ya kujifungua. Dkt. Tulyanje amesema upasuaji ulifanyika salama na wote walitoka salama na wazazi hao wanaendelea vizuri pamoja na watoto wao wakiwa na afya njema.
“wamama hao wote wawili walifanyiwa operesheni na madkatari pamoja na wauguzi katika hospitali yetu kwa mara ya kwanza na tukafanikiwa kutoka salama mpaka sasa hivi wanaendelea vizuri akina mama pamoja na watoto wao………” amesema Dkt. Tulyanje.
Aidha, Dkt. Tulyanje ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma ya afya na kuwapatia fedha za ukamilishaji wa miundombinu katika Hospitali hiyo.
“kimsingi tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za kukamilisha miundombinu, kutupatia vifaa tiba ambapo mpaka leo tumefanikiwa kuokoa maisha ya hao akina mama wajawazito na tutaendelea kutoa huduma ya namna hiyo……………….” Ameongeza Dkt Tulyanje.
Kwa upande wao, wanawake waliopatiwa huduma ya upasuaji katika Hospitali hiyo wameishukuru serikali kwa kuboresha huduma za afya katika maeneo yao jambo linalorahisisha upatikanaji wa huduma karibu nao wakatim wowote. Bi. Shamsia Salehe amesema ameridhishwa na huduma iliyotolewa na wahudumu wa afya katika hospitali hiyo kwakuwa alihudumiwa haraka.
“jopo la wauguzi waliofika tu kwanza walinifurahisha kwasababu walikuwa wakarimu, wachangamfu, huduma zilienda kwa wakati, muda huo huo saa tisa niliingizwa theatre kunifanyia operesheni, operesheni ilienda vizuri kwakweli nili enjoy, sijasikia maumivu ya aina yoyote……….” Ameongeza Bi. Shamsia Salehe.
Pamoja naye, Bi. Loveness Donasiano amesema kuwa amefurahishwa na uchangamfu wa wahudumu kwakuwa walijitoa haraka kuokoa maisha yao jambo lililomfanya ampe mwanae jina la Daktari aliyemhudumia.
“kwa jinsi walivyonifanyia vizuri wakanihudumia vizuri nimeamua kumwita jina la mhudumu aliyenihudumia anaitwa David……..” amesema Bi. Loveness Donasiano.
Huduma ya kujifungua kwa njia ya upasuaji imekuwa ya kwanza katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo tangu ilipoanza kutoa huduma za afya, jambo linalorahisisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi wa Nsimbo.

Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa