Pichani:(Katikati)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw Mohamed Ramadhani alipozungumza na walimu wakuu,wakuu wa Shule,Wafawidhi wa Vituo,Wakuu wa Idara na Vitengo,pamoja na Watendaji wa Kata wenye Miradi(Hawako pichani) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nsimbo 20, Aprili 2022.
Nsimbo-Mtapenda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani amewataka Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wanaosimamia miradi mbalimbali ya Ujenzi inayotekelezwa ndani ya mwaka wa fedha 2021/2022 kuacha visingizio na badala yake wahakikishe wanakamilisha miradi hiyo ndani ya muda uliopangwa.
Mkurugenzi Mohamed ametoa rai hiyo Katika kikao na Wakuu wa Shule,Walimu wakuu,Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya,Watendaji wa Kata wenye miradi pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nsimbo 20, Aprii 2022.
Amebainisha kuwa kutokamilika kwa miradi ndani ya muda uliopangwa kunasababishwa na baadhi ya Watendaji kutowajibika ipasavyo katika nafasi zao hali inayopelekea miradi mingi ya Serikali kuchelewa kukamilika wakati.
Amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa kwa wakati pindi wanapopatwa na chamgamoto kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuchukuliwa hatua madhubuti kutatua changamoto katika eneo husika kwa haraka zaidi.
Aidha Mkurugenzi Mohamed ameongeza kuwa tabia ya Baadhi ya Watendaji kutokuwa waaminifu na kutanguliza maslahi binafsi mbele nayo kwa sehemu kubwa inachangia kuzorotesha utekelezaji wa miradi Serikalini.
Kutokana na sababu hizo Mkurugenzi Mohamed amewaagiza Watendaji hao kuacha visingizio na badala yake kila mmoja awajibike ipasavyo katika nafasi yake ili kuhakikisha kuwa miradi yote iliyotengewa na kupewa fedha kukamilika mapema kabla ya Tarehe 30 Juni 2022.
Ameeleza kuwa endapo Watumishi wa Serikali watatekeleza majukumu yao kwa Uadilifu na bidii pamoja na kutanguliza maslahi mapana ya Taifa mbele itasadia kwa kiasi kikubwa kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maendeeo ndani ya muda uliopangwa jambo litakaloharakisha maendeleo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mohamed amewataka Watumishi hao kuepuka kufanya urasimu usiokuwa na lazima kwa kuwa kufanya hivyo kwa sehemu kubwa ndiko kunakoathiri utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na hivyo kupelekea kutokamilika kwa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa wakati.
Ametoa wito kwa Watalaamu hao kuhakikisha kuwa wanafanya maandalizi ya manunuzi ya Vifaa vya Ujenzi kwa wakati pamoja na kujiridhisha na ubora wakati wa manunuzi ili kuepuka kuleta sintofahamu zinazojitokeza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo.
Kwa Upande wao Walimu wakuu,Wakuu wa Shule pamoja na Watendaji wa Kata wenye miradi Nsimbo, wametaja sababu ya miradi kuchelewa kukamilika kuwa ni pamoja na baadhi ya mafundi wanaopewa kazi za Ujenzi kuzidiwa na kazi nyingi hali inayosababishwa na uhaba wa Mafundi Nsimbo.
Aidha wameitaja changamoto ya umbali kuwa sababu kubwa inayoathiri ukamilisha wa miradi kutokana na malighafi pamoja na vifaa vya Ujenzi kuwa mbali na eneo la Ujenzi huku wakitaja hangamoto ya Usafiri kuathiri Utekelezaji wa Miradi hiyo ya Ujenzi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa