Wakati watahiniwa wanaotarajia kufanya mtihani wao wa Taifa wa kuhitimu Kidato cha nne (CSEE) unaonza Novemba 17, 2025 hadi Disemba 5, 2025, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Daniel Bunini, menejimenti pamoja na watumishi wote wamewatakia mtihani mwema watahiniwa hao.
Katika Halmasahuri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, Jumla ya watahiniwa mia tisa sabini na tatu (973), kati yao wasichana wakiwa 501 na wavulana 472 wanatarajia kufanya mtihani huo wa Taifa wa kuhitimu kidato cha nne katika vituo kumi na tatu (13).

Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa