Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Daniel Bunini, amewatakia mtihani mwema watahiniwa wote wanaohitimu Elimu ya Msingi unaotarajia kufanyika tarehe 10-11 Septemba 2025.
Akizungumza na baadhi ya watahiniwa katika Shule ya Msingi Songambele iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, Bi. Christina Bunini amewataka watahiniwa hao kujiamini na kuondoa hofu katika katika kipindi chote cha ufanyikaji wa mtihani huo.
Aidha, amewataka watahiniwa hao kuwa na ujasiri na utulivu pamoja na kufuata taratibu zote zilizotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
“Kesho mnaanza mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi, fanyeni mtihani mkiwa na afya njema, mjiamini kwakuwa mmeshafundishwa vizuri na mko tayari kufanya mtihani. Mfuate taratibu zote za Baraza la Mitihani, Ninawatakia mtihani mwema”
Kwa upande wake, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo Mwalimu Frank Sichalwe amewataka wanafunzi kuwa watulivu, wenye ujasiri na kutokuogopa wasimamizi wa mitihani, kwani wao ni wasaidizi watakaohakikisha mitihani inafanyika kwa amani na utulivu.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Jumla ya watahiniwa 3,323 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi kati yao wasichana wakiwa 1,897 na wavulana 1,426 watakaofanya mtihani huo katika vituo 64.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa