Mkurugenzi Mtendaji Eng. Stephano B. Kaliwa aliwataka wajumbe kuhakikisha wanazingatia elimu inayotolewa juu ya lishe bora kwa maendeleo ya jamii. Aliyasema hayo wakati akifungua kikao muhimu cha Afya na Lishe, kilichofanyika kama sehemu ya vikao vya utekelezaji wa afua za lishe ya robo ya kwanza katika mwaka wa fedha 2024/2025.Kikao hicho kilifanyika kwa lengo la kutathmini na kujadili masuala ya afya na lishe ndani ya halmashauri.
Katika hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa wananchi kutumia mbinu za lishe bora ili kupunguza magonjwa yanayotokana na lishe duni, hasa kwa makundi maalum kama watoto, wajawazito na wazee
Afisa Lishe, akitoa mchango wake, alielezea hatua mbalimbali ambazo Halmashauri imechukua katika kuhakikisha kuwa elimu ya lishe inawafikia wananchi kwa ufanisi. Pia alitoa ushauri wa kitaalamu juu ya vyakula vinavyohitajika kuboresha lishe na kuimarisha afya. Alisisitiza kuwa lishe bora ni msingi wa jamii yenye afya njema na tija.
Wajumbe wa kikao hicho walipata fursa ya kuchangia maoni yao, ambapo walijadili mafanikio na changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa mpango wa afya na lishe. Baadhi walipendekeza mbinu za kuongeza ufanisi wa utoaji elimu ya lishe na afya kwa wananchi ili kuhakikisha wanapata uelewa mpana juu ya masuala hayo muhimu.
Mwenyekiti wa kikao, Mkurugenzi Mtendaji ,alihitimisha kwa kutoa wito kwa wote waliohudhuria kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu wa lishe. Alisema kuwa ushirikiano wa wananchi na wataalamu ni muhimu katika kufikia malengo ya afya bora na lishe katika Halmashauri ya Nsimbo.
Aidha,amesema kuwa elimu ya lishe pamoja na kutolewa shuleni bado ni muhimu kutolewa majumbani pamoja na vituo vya afya. Aliwataka madaktari na wadau wote wa afya kuhakikisha kuwa afya inachukuliwa kama agenda kuu na utekelezaji wake ufanyike haraka wakati wote bila kutoa sababu ambazo hazilingani na umuhimu wake.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa