Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Daniel Bunini amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wawakilishi kutoka shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) katika kujadili na kutathmini namna bora ya kuendeleza miradi inayofadhiliwa na shirika hilo na kuborehsa ujirani mwema kati ya shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Bi.Christina amewapongeza TANAPA kwa kudhamini miradi mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo ikiwemo mradi wa ujenzi wa shule ya sekodari Sitalike na kusema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kutaongeza chachu ya maendeleo katika wilaya hiyo kwani ni wazi kwamba shule hiyo itazalisha wasomi mbali mbali watakao kuja kuwa wazalishaji mali kwa maendeleo ya halmahauri ya nsimbo na taifa kiujumla.
Katika kuboresha ujirani mwema Bi. Bunini amesisitiza utolewaji wa elimu ya utunzwaji wa mazingira kwa wananchi wote wanoishi katika vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Nsimbo ambavyo vinapakana na hifadhi ya taifa ya Katavi ilikuwezesha wananchi hao kuweza kutunza mazingira ya hifadhi zetu na kuboresha mahusiano mema yaliyopo kati ya wanakijiji na shrika la hifadhi za taifa (TANAPA)
Pamoja na hayo Bi Christina Bunini ameonesha kufurahishwa na ushirikiano unaoendelea kati ya Halmashauri wilaya ya Nsimbo na TANAPA katika kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na Kijamii kwa pande zote mbiil ikiwemo utolewaji wa elimu ya ufugaji wa nyuki pamoja na ujenzi wa uzio wa kuzuia wanyama kushambulia mizinga ya Nyuki
Aidha Vijiji mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo vimepakana na hifadhi ya Taifa ya katavi ikiwemo kijiji cha Muungano kata ya Ibindi ambapo hali hiyo imekuwa ikitoa fursha ya kiuchumi kutokana na shughuri mbalimbali za kibiashara zinazoendelea katika maeneo hayo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa