Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilikadiria kukusanya kiasi cha Tsh. 1,021,980,000 na kutenga asilimia 10 ya mapato hayo ambayo ni Tshs 102,198,000 kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake, Vijana na watu wenye Walemavu.
Kwa awamu ya kwanza, Mwaka huu wa fedha Halmashauri imetoa mkopo wenye thamani ya Tshs 49,350,000 kwa vikundi 3 vya Vijana na vikundi 4 vya wanawake kutoka katika mapato ya ndani na hivyo kubakiza kiasi cha Tsh 52,848,000 ambazo zitatolewa Awamu ya pili mwezi Juni 2023.
Halmasahuri pia imetoa Tsh.99, 000,000 kutokana na fedha za marejesho ya vikundi kwa vikundi 9 vya Wanawake, kikundi 1 cha watu Wenye Ulemavu na vikundi 6 vya Vijana vyenye jumla ya wanachama 141, Hivyo kufanya jumla ya Tsh. 148,350,000. (Wanawake vikundi 13 Tshs. 68,900,000, Vijana vikundi 9 Tshs 70,450,000 na Watu wenye ulemavu Tsh. 9,000,000 kwa kikundi 1.
Katika halfa ya ugawaji mikopo hiyo Mgeni Rasmi Mhe. Anna Richard Lupembe (Mbunge wa jimbo la Nsimbo) amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kurejesha mikopo hiyo. Amesisitiza kuwa endapo vikundi vitashidwa kurejesha fedha hizo vitakuwa havijawatendea haki wakopaji wengine ambao wanakopa kutokana na fedha za marejesho ya mikopo hiyo. Pia Mhe. Mbunge amewashukuru vikundi vyote vilivyopata mkopo kwa mara ya pili au ya tatu na kusema kuwa kupewa kwao mikopo hiyo inaonesha uaminifu wao usio na shaka na hivyo kuwaomba waendelee kuwa waaminifu. Pia alisisitiza matumizi ya mikopo hiyo yafanyike kadri ya maandiko yao na si vinginevyo. Mh mbunge ameahidi kuendelea kuhamasisha uundaji wa vikundi vya vijana na kuwapa kipaumbele katika shughuli za maendeleo ya Halmashauri.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa