Katika kuendeleza juhudi za kuhakikisha ushiriki mkubwa wa wananchi katika zoezi la uandikishaji katika daftari la wapiga kura kuelekea uchaguzi wa viongozi wa serilali na vitongoji, Katibu Tawala akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Nsimbo pamoja na Afisa Maendeleo, amefanya ziara Nsimbo kuhakikisha zoezi la uandikishaji linaendelea kama ilivyopangwa.
Aitha katika ziara hiyo ilihusisha kutembelea vituo kadhaa vya uandikishaji, ambako kiongozi huyo alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wananchi waliokuwepo vituoni kujiandikisha na wale ambao hawajajiandikisha kufanya zoezi hilo kwani ni la muhimu, Alihimiza maafisa wasaidizi wa uchaguzi kuendelea na hamasa katika maeneo yao ili wananchi waweze kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha, akisisitiza kuwa zoezi hili ni la muhimu kwa maendeleo ya demokrasia nchini.
“Hakikisheni mnatumia fursa hii kujiandikisha ili muweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao," alisema kiongozi huyo wakati akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya ugalla baada ya kutembelea kituo cha uandikishaji kilichoko Kijiji cha katambike
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nsimbo alibainisha kuwa serikali imeweka mipango madhubuti kuhakikisha zoezi la uandikishaji linafanyika kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa.
Waandikishaji nao walionyesha shukrani kwa uongozi na kuahidi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo, wakisisitiza umuhimu wa ushiriki wao katika kujenga taifa.
Zoezi la uandikishaji linaendelea mpaka tarehe 20 October 2024 na wananchi wanaohimizwa ni wale ambao bado hawajaandikishwa au ambao taarifa zao zinahitaji kusasishwa
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa