Pichani:Watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiwemo wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa katika mafunzo ya Maandalizi ya mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwa ni maandalizi kuelekea shughuli hiyo.
Maafisa wa ngazi mbalimbali wakiwemo wakuu wa Idara na Vitengo waHalmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wamepatiwa Mafunzo ya Mfumo wa Mpango na Bajeti(PLAN REP) ikiwa ni maandalizi kuelekea utekelezaji wa shughuli ya kuandaa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2022/2023.
Mafunzo hayo yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI yalilenga kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Waandaaji wa Bajeti,Waganga wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya,Walimu wakuu wa shule pamoja na Watendaji wa Kata juu ya namna ambavyo wanapaswa kufanya maandaliz ya Bajeti kwa kuzingatia Miongozo mbalimbali inayohusika katika Uandaaji wa Bajeti ya Halmashauri.
Tayari Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imekwishaanza kufanya maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wanatekeleza shughuli hiyo muhimu kwa kuzingatia muda ili kuepuka kuchelewesha Bajeti hiyo jambo litakaloathiri kwa sehemu kubwa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Kimanendelea ndani ya Halmashauri.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa