Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Nsimbo limepitisha rasimu ya mapendekezo na mpango wa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 27 zimekadiriwa kukusanywa. Fedha hizo zinajumuisha mapato ya ndani pamoja na fedha kutoka Serikali Kuu, ambazo zitatumika katika utoaji wa huduma, utawala, na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Tukio hilo limefanyika katika Baraza Maalumu la Bajeti lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Nsimbo, ambapo Madiwani pamoja na wataalamu wa Halmashauri wamehudhuria na kujibu hoja mbalimbali wakati wa kujadili bajeti hiyo.
Baada ya mapendekezo ya bajeti hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Halawa Malendeja, amesema kuwa ukusanyaji wa mapato umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na ushauri mbalimbali unaotolewa na madiwani kuhusu vyanzo vya mapato vinavyopatikana ndani ya halmashauri hiyo.
Pamoja na kupitishwa kwa rasimu hiyo, Madiwani wameomba uzingatiwaji wa utoaji wa risiti rasmi katika ukusanyaji wa mapato ili kudhibiti upotevu wa mapato yanayokusanywa bila utaratibu. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ndugu Adolf Semindu, amewaomba Madiwani kushirikiana kwa pamoja kudhibiti mianya yote ya ukwepaji wa kodi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa