Pichani:Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakifuatilia kwa umakini rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2022/2023 ilipowasilishwa kikaoni hapo 20 Januari 2021
Na:John Mganga-DIO
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo limepitisha zaidi ya Shilingi Bilioni 20.6 ikiwa ni Rasimu ya Makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka mpya ujao wa Fedha 2022/2023 ikiwa na ongezeko la 0.98 ukilinganisha na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Akifungua Mkutano wa Baraza la Bajeti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Halawa Charles Malendeja amewapongeza wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kufanikisha maandalizi ya Rasimu hiyo kwa wakati.
Mkuu wa Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi.Victoria Cilewa Akiwasilisha Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa Mwaka mpya wa Fedha 2022/2023 amewaambia Wajumbe wa Baraza la Madiwani katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri kuwa makadirio hayo ni sawa na ongezeko la Asilimia 0.98 yakilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 ambayo ilikuwa Shilingi 20,668,252,869.00
Ameeleza kuwa kati ya kiasi hicho cha Fedha,Shilingi 10,106,187,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara,Shilingi 2,071,685,000.00 ni kwa ajili ya matumzi mengineyo ambapo Shilingi 7,917,500,850,00 imeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Katika rasimu hiyo ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 imeelezwa kuwa Halmashauri inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi 1,327,189,000.00 ambapo Shilingi 1,021,980,000.00 ni vyanzo visivyolindwa(Ownsource Proper) na Shilingi 305,209,000.00 ni kutokana na vyanzo lindwa.-Bima ya Afya,NHIF,Mfuko wa Afya ya Jamii CHF pamoja na User Fee.
Aidha katika Bajeti hiyo ya Shilingi 1,021,980,000.00 cha mapato ya ndani kilichoidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Asilimia 40 sawa na Shilingi 408,792,000.00 itatumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo Shilingi 613,188,000.00 sawa na Asilimia 60 imegawanya kwenye Idara kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Wajumbe wa Baraza la madiwani pamoja na ushauri wamepongeza Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kufanikisha maandalizi ya rasimu hiyo ya Bajeti kwa wakati.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Picha 1;Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Halawa Charles Malendeja alipofungua kikao cha Baraza la Madiwani kujadili Rasimu ya Bajeti mpya 2022/2023
Picha 2;Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakifuatilia kwa makini katika Majalada yao Rasimu ya Makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka mpya wa Fedha 2022/2023 ilipowasilishwa kikaoni hapo 20 Januari 2022
Picha 3;Mkuu wa Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi.Victoria Cilewa akiwasilisha Rasimu ya Mkadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka mpya ujao wa Fedha 2022/2023 katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Bajeti 20 Januari 2022/2023.
Picha 4;Diwani wa Kata ya Itenka alikuwa Miongoni mwa Wajumbe waliotoa Ushauri wakati wa kikao cha kujadili Rasimu ya Bajeti ya Mwaka mpya wa Fedha 2022/2023.
Picha 5;Raphael Kalinga,Diwani wa Kata ya Mchimboni akiwasilisha mchango wake baada ya Rasimu ya Bajeti mpya kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kuwasilishwa mbele ya Madiwani.
Picha 5;Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiwa katika Kikao cha Barza la Madiwani kujadili Rasimu ya Bajeti mpya 2022/2023
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa