Mkuu wa Wlaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Mhe. Jamila Yusuph amekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 300 kwa vikundi 37 Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Hafla hiyo imefanyika Oktoba 27, Katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msaginya. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni muendelezo w mpango wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alieagiza kila Halmashauri nchini kutenga 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Walemavu.
Mhe. Jamila wanufaika wa fedha hizo kuhakikisha wanazitumia katika malengo na utaratibu waliyojiwekea awali. "Tunawapa fedha hizi kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais, kazifanyieni kazi ili zijizalishe mpate kufanya marejesho na wenzenu nao wapate na hilo ndio lengo kuu la Serikali"
"Ikitokea umepata chanagamoto msijifungie ndani, msiwaze mawazo mabaya sisi ndio walezi wenu njooni ili tuweze kujua tunawasaidiaje, kukimbia sio suluhisho ni kujitafutia tu matatizo"
"Vijana msibabaike na fedha hizi, mkituliza akili na kujikita kwenye malengo yenu mna uwezo wa kuzalisha pesa zaidi ya hizi"
Mbali na Mhe. Jamila, Wanufaika hao pia walipata semina elekezi kutoka kwa Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii kutoka H/W ya Nsimbo, Bwana Rodrick Kidenya ambae aliwapa somo namna ya kuhakikisha mikopo hiyo wanayopewa inaleta tija kwao na taifa kwa ujumla.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa