Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeendelea kusimamia na kutekeleza utoaji wa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Vijana kwa tamko la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa kifungu 17(1) cha Sheria ya Excheque and Audit Ordinance (Cap 439) ya mwaka 1961 pamoja na maboresho yake na kwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo ya kutenga fedha kutoka katika mapato yake ya ndani na kupeleka katika Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ilikadiria kukusanya kiasi cha Tshs. 1,000,098,000 na kutenga asilimia 10 ya mapato hayo ambayo ni Tshs 100,098,000 kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu.
Hadi kufikia tarehe 30 Mwezi Mei 2022, Halmashauri imeshakusanya kiasi cha Tshs 1,092,480,889 ya Mapato yake ya ndani ambayo ni asilimia 109 ya lengo, hivyo mpaka sasa Halmashauri ilitenga kiasi cha 109,248,088.90 kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu ili kuwezesha Mfuko wa Mkopo utoe mikopo kwa Walengwa ambazo zimetolewa kwa awamu mbili.
Kwa awamu hii ya mwisho wa mwaka huu wa fedha Halmashauri imekusudia kutoa mkopo wenye thamani ya Tshs 30,000,000 kwa vikundi 2 vya Vijana kutoka katika mapato ya ndani Tshs. 79,000,000 kutokana na fedha za marejesho ya vikundi kwa vikundi 7 vya Wanawake na kikundi 1 cha watu Wenye Ulemavu, vyenye jumla ya wanachama 68. Hivyo kufanya jumla ya Tshs. 109,000,000. (Wanawake vikundi 7 Tshs. 39,000,000, Vijana vikundi 6 Tshs 68,000,000 na Watu wenye ulemavu Tshs. 2,000,000 kwa kikundi 1.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa