Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Nsimbo amewataka wanafuzi wa kidato cha nne kufanya mitihani yao katika hali ya utulivu kwa kuzingatia maadili ili kupata matokeo bora ambao yatajenga msingi mzuri kwa elimu yao ya juu na kwa mustakabali wao wa maisha ya baadaye
‘’ Ninawatakia kila la kheri kwenye mitihani yenu. Huu ni wakati wa kuonyesha matunda ya bidii na juhudi mlizoweka katika masomo yenu. Kumbukeni mtihani ni ni kipimo cha yale mliyofundishwa na kujifunza, kuweni, kila mmoja wenu ana uwezo wa kufanya vizuri fanyeni kila swali kwa umakini mafanikio yenu yanategemea nidhamu,utulivu, na juhudi zenu. Tunawaamini na tuna Imani mtang`ara’’
Mkurugenzi ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliokua wakijiandaa kwa mitihani hiyo. Aidha amesema kua wazazi, Walezi pamoja na Waalimu wanapaswa kuwapa wanafunzi ushirikiano mzuri katika kipindi hiki cha mitihani ambapo takribani wanafunzi mia nane arobaini na nane, wakiwempo wavulana 405 na wasichana 403 wanatarajiwa kufanya mitihani. Halamshauri ya Nsimbo Ina jumla ya shule Kumi na Nne (14) zinazotarajiwa kufanya mitihani hiyo ya Kitaifa.
Mitihani ya kidato cha nne ni hatua muhimu katiak mfumo wa elimu nchini Tanzania huamua kama mwanafunzi ataendelea katika na masomo ya juu zaidi ama program nyingine za mafunzo
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa