Katika kuimarisha afya ya mwili na akili pamoja na kudumisha mshikamano, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ameongoza mazoezi ya pamoja ya jogging yaliyofanyika leo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Nsimbo.
Mazoezi hayo yameshirikisha watumishi wa Halmashauri pamoja na wananchi kutoka maeneo ya jirani, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhamasisha maisha yenye afya na kuongeza ushirikiano baina ya serikali na jamii.
Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Mkurugenzi alisema kuwa lengo ni kuimarisha afya na kuondoa magonjwa ya mwili,kuongeza mshikamano na upendo kati ya watumishi na wananchi, pamoja na kuchochea ari ya kufanya kazi kwa tija.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa wanafunzi wa shule za jirani kushiriki katika mazoezi hayo, akibainisha kuwa ni njia bora ya kuimarisha afya ya akili na kupunguza msongo wa mawazo (stress), hali itakayowasaidia kusoma kwa utulivu na kuongeza ufaulu.
Akiongoza mazoezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji alisisitiza pia umuhimu wa kufanya mazoezi mara kwa mara kama njia ya kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na kuboresha utendaji kazi. “Afya njema ni msingi wa maendeleo. Tunapokuwa na afya bora, hata huduma kwa wananchi huimarika,” alisema.
Wananchi na watumishi waliohudhuria walionekana kufurahishwa na tukio hilo, wakieleza kuwa ni hatua chanya inayopaswa kuendelezwa ili kuimarisha afya, mshikamano na ushirikiano ndani ya jamii.
Mazoezi haya yanatarajiwa kufanyika kila wiki, yakihusisha makundi mbalimbali ya jamii, huku wakazi wengi wakionekana kuwa na hamasa kubwa ya kushiriki mara kwa mara.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa