Mkuu wa Wilaya Bi Jamila Yusufu Kimaro amezindua rasmi mradi wa Uboreshaji wa Miundombunu ya Barabara katika Halmashsuri ya Nsimbo. Mradi huo unahusisha uboreshaji wa barabara za Ikondamoyo – Mihambo Usense Km 6.0, Urwira – Mission B Km 6.0, Songambele – Mkumbi Road Km 5.0 na Nyati Km 1.5, pamoja na Ujenzi wa Daraja la Upinde la Mawe katika barabara ya Ikondamoyo – Mihambo – Usese na Ujenzi wa Makaravati kwenye Barabara Za Urwira – Mission B (5), Songambele – Mkumbi Road (5) Na Barabara Ya Nyati (3).
Akizungumza katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya alieleza umuhimu wa barabara hiyo kwa maendeleo ya kijiji, akibainisha kuwa mradi huo ni sehemu ya mikakati ya serikali ya kuimarisha miundombinu vijijini Alisistiza kua barabara hiyo itachochea uchumi wa wananchi kwa kurahisisha usafiri na biashara. Vilevie alimpongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha, nyingi kwa ajili ya mradi huu ambapo kila mtu anaona kwa macho serikali sikivu yenye kujali wananchi wake.
Aidha Mkuu wa Wilaya Aliongeza kua Serikali imeendelea kuweka kipaumbele katika kuboresha maisha ya wananchi, hususan katika maeneo ya vijijini, na amekiri TARURA kupokea kiasi cha Sh 838’426’765.00 kwa ajili ya mradi huo Aliongeza kua hadi kufikia tarehe 29/04/2025 ikiwa ni miezi sita tangu kuanza kwa mradi huo, uwe umekamilika
Katika hatua nyingine muhimu Mkuu wa wilaya alisaini mkataba wa ujenzi na kukabidhiwa rasmi kwa mkandarasi atakayesimamia mradi huo ambapo Katika tukio hilo, alimkabidhi cheti rasmi cha kutekeleza mradi huo.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa wilaya aliambatatana na viongozi wa chama,Madiwani afisa Tarafa. Viongozi hawa walitoa shukrani za dhati kwa serikali kwa jitihada zake za kuboresha miundo mbinu. Na kusistiza wananchi kushirikiana vizuri na Mkandarasi ili kufanikisha mradi huo.
Kwa upande wa ajira za vijana, Mkuu wa Wilaya alitoa wito kwa vijana wa kijiji kushiriki kikamilifu katika kazi za ujenzi wa mradi huo kwa uaminifu na bidii. Alisema kwamba ajira hizo ni fursa muhimu kwa vijana kujiendeleza kiuchumi, na aliwasihi kufanya kazi kwa uwajibikaji ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo kwa viwango vya juu. na kwa wakati
Akizungumza kuhusu mchakato wa uchaguzi, Mkuu wa Wilaya aliwakumbusha wananchi kuhusiana na uchaguzi kwa kusema kua,‘’zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi limekamilika, na sasa ni muda wa kuelekea kwenye uchaguzi wenyewe. Mnapaswa kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo kwa vitendo badala ya kupelekwa na maneno matupu ya wagombea. ninyi wenyewe ni mashuhuda wa maendeleo yanayofanywa na serikali’’ alisema haya akisisitiza umuhimu wa kuchagua kwa busara na kwa kuzingatia uwezo wa mgombea kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma’’.
Aidha msimamizi wa mradi huo ambaye na meneja wa TARURA Mpanda, wakati wa kuwasilisha mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo aleleza mkataba huo unaweka misingi wa utekelezaji wa mradi na kwa kuzingatia manunuzi ya serikali ambappo mkataba huo ulisainiwa na mkuu wa wilaya mbele ya washiriki wa mkutano huo. Alitoa wito kwa Mmkandarasi kuhakikisha kwamba ujenzi unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika ili kulinda thamani ya fedha za umma kama zilivyotolewa kwenye mradi huo.
Nae mkandarasi aliyejulikana kwa jina M/S/SABD COMPANY LMTD aliyekabidhiwa mradi huo alishukuru serikali kwa kuendelea kumuamini aliwaomba wananchi kwa ushirikiano na kuwataka wawe kipaumbele katika kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kisha alimpongeza Rais Samia kwa kutoa kipaumbele kwa miundombinu. Aliahidi kufanya kazi kwa kasi na ubora ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi wote.
Wananchi walionyesha shukrani zao kwa serikali kwa kuwajali na kuwaletea maendeleo, huku wakiahidi kushirikiana kikamilifu na mkandarasi ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa mafanikio.makubwa.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa