Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo amekutana na viongozi wa vyama vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 kwa lengo la kujadili utaratibu utakaotumika wakati wa uchaguzi. Vyama vilivyoshiriki mkutano huo ni CCM, CHADEMA, ACT WAZALENDO, CUF, UDP, UMD, NCCR MAGEUZI na ADC. Katika mkutano huo, msimamizi wa Uchaguzi:-
Aidha, katika mkutano huo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pia ilitoa elimu ya rushwa kwa vyama na wagombea, ikisisitiza madhara ya rushwa katika mchakato wa uchaguzi. Afisa wa TAKUKURU Bw Leonald J.Minja, alibainisha kuwa vitendo vya rushwa vinaweza kupunguza uadilifu katika uchaguzi, kuvuruga demokrasia, na kupelekea kuchaguliwa kwa viongozi wasiowajibika kwa wananchi.
Aliwahimiza wagombea na wafuasi wa vyama kuwa mstari wa mbele kupinga rushwa na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapoona vitendo vya rushwa vinavyojitokeza. Aidha, alitoa onyo kali kwa wale wanaopanga au kushiriki katika vitendo vya rushwa kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi. Aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huu kwa uadilifu na uwazi, bila kuacha nafasi kwa rushwa kuvuruga mchakato wa kidemokrasia.
Aitha Msimamizi wa uchaguzi amewaomba viongozi wa vyama kuhakikisha wanaendelea kuhamasisha wananchi wajiandikishe kwenye daftari la mkazi na mwisho ametoa wito kwa wananchi wote kushiriki kwa wingi na kwa amani katika zoezi hili muhimu la kidemokrasia ili kuchagua viongozi bora watakaowakilisha maslahi yao.
SERIKALI ZA MITAA, SAUTI YA WANANCHI, JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa