Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Jamila Yusuph Kimaro akizungumza katika Mkutono wa Hadhara kueleza mafanikio ya Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan katika eneo la Dipacha Kijiji cha Ndui Stesheni Kata ya Katumba 18 Machi 2022.
Nsimbo- Katumba
Katika Kipindi cha Mwaka mmoja wa Utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imepata mafanikio makubwa na ya kihistoria katika sekta mbalimbali Viongozi wa Wilaya wameeleza.
Kwa nyakati tofauti 18 Machi 2022 Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Jamila Yusuph Kimaro alipozungumza na Wananchi wa Kata za Sitalike Kijijini Magula na Katumba Kijjini Ndui Stesheni amewaambia Wananchi kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Utawala wa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imepata mafanikio makubwa kuwahi kutokea katika hitoria ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
DC Jamila amewaambia Wananchi wa Kata ya Katumba Nsimbo katika mkutano wa hadhara kuwa katika kipindi cha Mwaka mmoja ukiacha Halmashauri nyingine Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo peke yake imepokea zaidi ya Shilingi Bilioni 6.
Ameeleza kuwa Fedha hizo zimeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Ujenzi wa miundombinu ya Elimu kama vile Vyumba vya Madarasa,Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati,pamoja na uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Kwa Upande wa Mapato ya ndani Mh Jamila pia amewaeleza Wananchi kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo hadi kufikia Februari imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 800 za mapato ya ndani ambapo Asilimia 40 ya makusanya hayo ya mapato ya ndani zimeelekezwa kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Aidha DC Jamila ameeleza kuwa Mh.Rais Samia alielekeza na kuhimiza utengaji wa Asilimia 10 kwa ajili ya kuwawezesha akina mama,Vijana na Watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa Fedha zilizokusanywa kama ushuru kwa wananchi zinarudi kwa Wananchi hao kuteleleza miradi mbalimbali ambapo hadi kufikia Mwezi Februari Halmashauri imeendelea kutumia fedha za Asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kuwawezesha wau wa makundi hayo maalumu.
Kutokana na Mafanikio hayo yaliyopatikana katika kipindi cha awamu ya sita ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkuu huyo wa Wilaya alitoa rai kwa Wananchi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika kuchangia nguvu kazi katika miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa.
DC Jamila ametoa rai kwa Wananchi kulinda miradi mbalimbali iliyoanzizhwa na kutekelezwa na Serikali ili kusudi ilete manufaa yaliyokusudiwa na Wananchi waweze kunufaika vema na miradi hiyo huku akiwasihi Wananchi kudumisha Amani na utulivu.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi Tabia Nzowa kwanyakati tofauti alizungumza na Vyombo vya Habari kueleza Mafanikio ya Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia.
Bi Tabia alipozungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Mkoa Wa Katavi wakati wa ziara yake kutembelea miradi iliyotekelezwa na Rais Samia kwa kipindi cha Mwaka mmoja ikiwa ni maandalizi ya Makala ya utekelzaji wa miradi hiyo alieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imepata bahati kubwa ya kupokea fedha nyingi zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Tabia amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi cha Mwaka mmoja tangu aingie madarakani huku akiahidi kwa niaba ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kusimamia vema utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kuhakikisha kuwa miradi inayoendelea kujengwa inakamilika kwa wakati,viwango na kwa muda uliopangwa.
Kwa upande wao Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo pia wamemshukuru Rais Samia huku wakimtakia mafanikio mema katika utekelezaji wa majukumu yake mazito ya kuliongoza Taifa la Tanzania.
Mh.Rais Samia aliapishwa Rasmi 19 Machi 2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki Dunia 17 Machi 2021.
Pichani:Wananchi wa Kata ya Katumba wakimsikiliza aMkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Jamila Kimaro wakati wa Mkutano wa hadhara wa kueleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa