Pichani Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Mkoani Katavi Bw.Hosea Cheyo akizungumza na Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Nsimbo alipowatembelea Wanafunzi hao 17 mACHI 2022.
Nsimbo -Mtapenda
Mwandishi Mkongwe wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Mkoa wa Katavi Bw. Hosea Cheyo ametoa wito kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nsimbo kujitokeza kwa wingi kusomea taaluma ya Uandishi wa Habari .
Mwandishi Hosea Cheyo ametoa rai hiyo 17 Machi 2022 alipowatembelea Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nsimbo katika shughuli ya kuandaa Makala ya Mafanikio ya Mwaka mmoja wa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
Akizungumza na Wanafunzi hao alipopewa fursa ya kuwasalimia Mwanahabari Cheyo aliwataka Wanafunzi hao kutumia Fursa waliyopata kusoma kwa bidii ili waweze kuwa na uwezo wa kujikwamua na maisha.
Mwanahabari huyo mkongwe amewaeleza Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nsimbo kuwa Taaluma ya Uandishi wa Habari ni taaluma pana inayomfanya mtu kuwa na uelewa wa mambo mengi na hivyo kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kusomea Taaluma hiyo ili waweze kuisaidia Jamii ya Watanzania.
Hosea Cheyo ametembelea Shule ya Sekondari Nsimbo akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Nsimbo pamoja na Mtalamu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakati wa Maandalizi ya Makala ya mafanikio ya Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa