Pichani:Naibu Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Habari Utamaduni Wasanii na Michezo Mh.Pauline Gekule akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kanoge 13 Septemba 2021
Naibu Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Habari Utamduni Wasanii na Michezo Mh.Pauline Gekule amempongeza Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe kwa jitihada mbalimbali anazofanya kuinua Sekta ya Michezo ndani ya Halmashauri.
Mh.Gekule ametoa pongezi hizo alipozungumza na Wananchi wa Kata ya Kanoge Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika Shughuli ya kukabidhi Vikombe na zawadi mbalimbali kwa Washindi waliofuzu Ligi ya Anna Lupembe ambapo timu 132 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo zinashiriki katika ligi hiyo katika ngazi mbalimbali ambapo pia timu 28 za mpira wa Miguu za Wavulana na Wasichana kwa Shule za Sekondari zimezinduliwa kushiriki katika Ligi ya kuwania Kombe la Anna Lupembe kwa Shule za Sekondari
Naibu Waziri Gekule amewaambia Wananchi wa Kata ya Kanoge Nsimbo kuwa kuanzishwa kwa Ligi ya Kombe la Anna Lupembe kumesaidia kwa sehemu kubwa kuibua vipaji mbalimbali katika Michezo na hivyo kuifanya Sekta ya Michezo Nsimbo kupiga hatua kubwa kimaendeleo,ambapo amewataka Wananchi pamoja na Wadau mbalimbali wa michezo Mkoani Katavi kuiga mfano wa Mh.Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe katika jitihada za kuinua Michezo Nchini
Awali katika Kikao na Maafisa Habari Utamaduni na Michezo wa Mkoa wa Katavi Naibu Waziri Gekule ameeleza kuwa anatambua changamoto ya uhaba wa watumishi katika Kada za Michezo utamaduni na Habari ambapo amehimiza uwajibikaji kwa waliopo ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Wasanii Utamaduni na Michezo Katavi inaendelea huku akiahidi kutatua changamoto ya Uhaba wa Mafaisa Michezo na Utamaduni mkoani humo.j
Akitoa salamu kwa Wananchi mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe amesema lengo la Ligi hiyo ni kuibua vipaji na kuleta ari ya Michezo ndani ya Halmashauri jambo litakalosaidia kwa sehemu kubwa kuibua vipaji mbalimbali vya Wanamichezo katika Jimbo lake.
Mh.Lupembe amemuambia Naibu Waziri Pauline Gekule kuwa kuanzisha Ligi hiyo katika Halmashauri imetokana na Halmashauri kuwa nyuma katika michezo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa Maafisa Utamaduni na Maafisa Michezo jambo ambalo limekuwa likiathiri kwa sehemu kubwa uratibu wa Ligi mbalimbali Nsimbo.
Amesema kuanzishwa kwa Ligi ya Anna Lupembe ni utekelezaji wa kile alichokiahidi wakati akiinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu Sekta ya Michezo na kwamba Wananchi watarajie yote yaliyoahidiwa katika Sekta hiyo ya michezo yatatekelezwa.
Aidha Mh.Mbunge Lupembe amesema Ligi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu baadhi ya Wachezaji wenye vipaji vikubwa walioibuliwa katika Ligi hiyo wameweza kuchukuliwa kwenda kushiriki michuano katika sehemu mbalimbali nje ya mkoa wa Katavi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani amempongeza Mbunge wa Nsimbo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza sekta ya Michezo ndaniya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Zawadi mbalimbali ikiwemo Mipira na Jezi pamoja na Makombe vyenye thamani ya Shilingi Milioni tatu zimetolewa kwa Washindi mbalimbali walioshiriki na kufuzu Ligi hiyo ya Kombe la Anna Lupembe
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa