Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Hoza Mrondoko(Kulia mwenye kilemba chekundu) akizundua moja kati ya vyumba 87 vya Madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Sitalike Mradi ambao umekamilika kwa asilimia 100 hadi kufikia Desemba 31 2021.
Na:John Mganga DIO
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kusimamia kikamilifu na kufanikisha Utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa kupitia Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Mh.Mrindoko ametoa pongezi hizo katika Hafla ya Uzinduzi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Sitalike kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kukamilisha Ujenzi kwa asilimia 100 vyumba vya Madarasa 87 pamoja na kukamilisha Utengenezaji wa Madawati 470,pamoja na viti na meza 1153.
Katika Taarifa yake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati wa Hafla ya kukabidhi miradi hiyo,ilieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ilipokea Shilingi 1,740,000,000.00 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba 87 vya Madarasa katika Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari ambapo Ujenzi huo ulikamilika kwa asilimia 100 hadi kufikia 31 Desemba 2021.
Mkurugenzi Mohamed alieleza kuwa kwa sekta ya Elimu Sekondari Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 860,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 43 vya madarasa katika shule 12 za sekondari pamoja na utengenezaji wa viti na meza 2,150 ambapo kwa sekta ya Elimu Msingi Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 880,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 44 vya madarasa katika vituo shikizi 11 pamoja na utengenezaji wa madawati 660.
Kiasi cha Shilingi Milioni Thelathini na Saba Mia Saba Ishirini na Saba Elfu, Mia nne sitini na mbili (37,727,462.05) kimebaki ikiwa ni kwa ajili ya fedha ya matazamio za mafundi Tshs. 18,878,098.00, utengenezaji wa madawati ni Tshs. 12,506,525.00 na malipo ya vifaa vilivyoongezeka ni Tshs. 6,342,839.05.
Aidha Halmashauri imebakiwa na vifaa vyenye thamani ya Tshs. 29,117,000.00 ambavyo baadhi vitatumika kujengea vyoo katika vituo shikizi ili shule ziweze kusajiliwa na baadhi vitabadilishwa ili kugharamia utengenezaji wa madawati, viti na meza kwa shule ambazo hazijakamilisha.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Picha 1:Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya UVIKO 19 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Hoza Mrindoko 10 Jaanuari 2022
Picha 2;Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko kwa kutambua mchango wake wa usimamizi makini wa miradi ya UVIKO 19.
Picha 3; Mmoja wa wakuu wa Shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kenswa Aidan Killo akipokea Cheti cha kutambua Mchango wake wa usimamizi makini wa miradi ya UVIKO 19
Picha 4;Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Salehe Msompola akipokea cheti cha kutambua mchango wa usimamizi makini wa Miradi ya UVIKO 19 kwa niaba ya Mwenyekti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Halawa Charles Maelendeja.
Picha 5;Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko akitoa hotuba wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Madarasa ya UVIKO 19 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa