Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya Nsimbo, ametangaza rasmi kuanza kwa zoezi la kujiandikisha kwa wapiga kura katika uchaguzi ujao wa Viongozi wa serikali ya vijiji na vitongoji hapo tarehe 27/11/2024. Akiwa katika kituo cha Ofisi ya kijiji cha Isinde kitongoji cha Ikulu Amesema kuwa amejiandikisha mwenyewe kama ishara ya kuhamasisha wananchi wote wenye sifa kufika vituoni na kushiriki kikamilifu katika zoezi hili.
Msimamizi wa uchaguzi amesisitiza kuwa umuhimu wa wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuhakikisha kuwa wamejiandikisha mapema ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi ujao. "Kujiandikisha ni hatua muhimu kwa kila raia anayetaka kushiriki katika uchaguzi. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha tunapata haki ya kupiga kura kwa kujiandikisha mapema," aliongeza kua hamasa bado inaendelea na vituo vyote viko vizuri na zoezi hili halichukui muda mrefu ambapo baada ya kujiandikisha bado wananchi wanaweza kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Aidha ametoa ufafanuzi kua zoezi hili limeanza rasmi leo na litaendelea kwa muda wa siku 10 hadi tarehe Tarehe 21/10/2024]. Vituo vya kujiandikisha vipo wazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni kila siku, na wananchi wanahimizwa kufika mapema ili kuepuka msongamano wa siku za mwisho.
Wakati huohuo, msimamizi wa uchaguzi ameweka wazi kwamba wale ambao tayari wamejiandikisha wanapaswa kuhakiki taarifa zao na kufanya marekebisho yoyote yanayohitajika kipindi orodha itakapowekwa wazi.
Serikali inatoa wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha uchaguzi huru, haki, na wenye uwazi.
SERIKALI ZA MITAA, SAUTI YA WANANCHI, JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa