Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kapalala inayojengwa kwa Ufadhili wa Fedha za Mpango wa kuinua Ubora wa Elimu ya Sekondari Nchini SEQUIP unaoendelea katika Kata ya Kapalala Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo uko katika hatua nzuri na ya kuridhisha kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mhandisi Martin Kasonso ameeleza.
Mhandisi Kasonso ameeleza kuwa hadi kufikia 17 Machi 2022 Majengo yote yalikuwa katika hatua ya Upigaji wa lipu huku baadhi ya majengo yakiwa katika hatua ya ufungaji wa Dari ambapo mafundi wote waliopewa kazi hizo wanaendelea na shughuli za Ujenzi pasi kuwepo na changamoto yoyote iliyojitokeza
Katika utekelezaji ratiba ya ufuatiliaji wa karibu wa miradi mbalimbali inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi Tabia Nzowa 16, Machi 2022 alitembelea mradi huo ambapo alithibitisha maendeleo mazuri ya Ujenzi.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kapalala katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo unaotekelezwa kwa fedha za Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari Nchini SEQUIP T unahusisha Vyumba Nane vya Madarasa,Maabara tatu,Jengo la Utawala,Maktaba moja,Chumba cha TEHAMA pamoja na matundu Ishirini ya Vyoo
Serikali kupitia mpango wa kuinua Ubora wa Elimu ya Sekondari SEQUIP T ilitenga Kiasi cha Shilingi Milioni 600 kwa ajili ya Ujenzi wa Sekondari hiyo ya Wasichana ambapo hadi sasa Shilingi Milioni 470 zimekwisha tolewa kwa ajili ya kutekeleza Mradi huo unaotarajiwa kukamilika ifikapo Tarehe 08, Agosti 2022.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa