Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imekua ikitekeleza afua mbalimbali za Lishe kwa kufuata mwongozo wa Taifa wa Lishe, Mpango jumuishi wa Taifa wa pili (2021/2022-2025/26) pamoja na sera mbalimbali za nchi zinazolenga kuzuia na kupambana na Udumavu na Utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miaka 5. Pia kuzuia na kupambana na matatizo yatokanayo na ulaji usiofaa kwa watu wazima kama vile Saratani, Kisukari, Magonjwa ya mfumo wa damu (Cardiovascular diseases) na Shinikizo la damu hasa katika maeneo yale ya kipaumbele yaliyopo katika mkataba wa lishe ngazi ya Halmashauri, Kata na kijiji.
Katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri imefanya shughuli za usimamizi elekezi ambazo ni kuangalia utoaji wa Elimu ya Lishe katika vituo vya kutolea Huduma za Afya, Utambuzi na Matibabu ya Utapiamlo Mkali, utumiaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu na Upimaji wa hali ya Lishe kwa Watoto wa chini ya miaka Mitano.
Sanjari na hayo, umefanyika pia uhamasishaji wa utoaji wa chakula shuleni kupitia mikutano ya Hadhara iliyoendeshwa na watendaji wa vijiji na Kata ambapo wazazi walielezwa faida za wanafunzi kupata chakula shuleni na jinsi itakavyosaidia kupunguza utoro, uachaji shule na namna itakavyosaidia kukuza kiwango cha ufaufalu kwa wanafunzi. Pia afisa Lishe wa Halmashauri ya Nsimbo ametembelea Shule ya sekondari Mkaso, na Shule za Msingi za Isanjandugu, Songambele na Nsimbo kuhamasisha uanzishwaji wa klabu za Lishe katika shule hizo ili wanafunzi hao wafahamu Lishe bora na umuhimu wa kula vyakula mchanganyiko ili waweze kuwa mabalozi wa Lishe bora kwenye jamii na familia zao.
Aidha Halmashauri kupitia Sehemu ya huduma za lishe kwa kushirikiana na kitengo cha mawasiliano serikalini kimeendelea kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kufikisha Elimu ya Lishe kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kuandaa Makala laini na ngumu za lishe pamoja na vipeperushi vya makundi matano ya vyakula na kuvisambaza kupitia tovuti ya Halmashauri na mitandao ya kijamii, pia kutumia radio zilizopo Mkoa wa Katavi kutoa elimu ya Lishe bora.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa