Mkurugenzi Mtendaji Eng. Stephano B. Kaliwa amewaagiza wachimbaji kuondoka mara moja katika maeneo ya mto na kuacha kabisa shughuli za uchimbaji ndani ya mita 60 za mto pia amewasisitiza kufuata taratibu za uchimbaji kwa kuhakikisha uhifadhi wa mazingira na upatikanaji endelevu wa maji safi kwa jamii kwani uharibifu wa vyanzo vya maji ni tishio kubwa kwa maisha ya wananchi na viumbe hai wengine wa eneo hilo na kwa mustakabali wa rasilimali za maji. Aliyasema hayo wakati alipofanya ziara katika Kijiji cha Kapanda kata ya Machimboni kukagua shughuli za uchimbaji wa madini.
Akiwa kwenye ziara hiyo, alibaini kuwa wachimbaji walikuwa wakiharibu vyanzo vya maji kwa kufanya shughuli za uchimbaji ndani ya mita sitini (60) za mto jambo ambalo ni kinyume na taratibu za uhifadhi wa mazingira. Ingawa wachimbaji hao wanayo leseni halali za kufanya shughuli za uchimbaji, ameleza kuwa kwa kufanya hivyo wanavunja sheria kwa kuendesha shughuli zao katika maeneo ya vyanzo vya maji. Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji alielekeza wachimbaji wasiofata utaratibu wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004
Ziara hiyo ni moja kati ya ziara za kiutendaji zinazofanywa kwa nia thabiti ya kuthibiti, kusimamia na kuimarisha rasilimali asilia na kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinafanywa kwa kufuata sheria na kulinda mazingira.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa