Kamishna wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Asina Omary, amewataka wananchi wa Jimbo la Nsimbo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
"Ni muhimu kila mmoja ahakikishe anahakiki taarifa zake au anajisajili upya pale inapohitajika, ili asikose haki ya kushiriki uchaguzi," amesema Omary, mara baada ya kutembelea na kujionea namna zoezi hilo linavyoendelea katika baadhi ya vituo vya uandikishaji vilivyopo Nsimbo.
Kwa upande wao, Maafisa Uandikishaji wa Jimbo la Nsimbo wamesema kuwa zoezi hilo pia linafanyika kwa lengo la kuondoa kwenye daftari wale wasiostahili kuwepo tena, wakiwemo waliofariki au waliopoteza sifa za kisheria.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Jimbo la Nsimbo limeanza rasmi leo na linatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 7 mwaka huu.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa