Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko akizungumza na wazee maarufu na viongozi wa Dini wa Mkoa wa Katavi aliokuwa ameambatana nao alipotembelea Shule ya ya Sekondari Uruwira kukagua Madarasa ya UVIKO 19 yaliyokabidhiwa 10,Januari 2021.
Na; John Mganga -DIO
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka Wazee Maarufu na Viongozi wa Dini Mkoani Katavi, kuwa mabalozi kwa Wananchi katika kutangaza mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Samia ikiwemo mafanikio yaliyopatikana kutokana na fedha zilizotolewa kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo 13 Januari 2022 katika Ziara yake akiambatana na Viongozi wa Dini na Wazee maarufu wa Mkoa wa Katavi kukagua Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari Uruwira katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Mh.Mrindoko amewaambia Wazee maarufu na viongozi wa Dini kuwa, Mkoa wa Katavi katika kipindi kifupi cha awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kufufua uchumi katika Sekta mbalimbali Nchini ulioathirika kutokana na mawimbi kadhaa ya Janga la UVIKO 19, mkoa umepokea zaidi ya Shilingi Bil 32 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 425 katika Shule za Msingi na Sekondari,Vituo Shikizi,Utengenezaji wa Viti na meza pamoja na Uboreshaji wa miundombinu katika Sekta ya Afya.
Aidha Mh.Mrindoko amewapongeza Viongozi mbalimbali walioshiriki katika usimamizi mpaka kumaliza Ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo pia amewataka kutumia muda aulioaki kuhakikisha kuwa Wanahamasisha wazazi kuwaandikisha watoto wenye sifa za kujiandikisha Darasa la awali ili waweze kupata haki yao ya Elimu kwa kuwa Serikali imetekeleza kikamilifu wajibu wake wa kuhakikisha uwepo wa Vyumba vya madarasa pamoja na madawati.
Wakizungumza mara baada ya kukagua Vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari Uruwira vilivyojengwa kupitia fedha za UVIKO 19 vyenye thamani ya Shilingi Mil.80, viongozi mbalimbali wa dini pamoja na Wazee maarufu wa Mkoa wa Katavi wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa namna ambavyo imesimamia Ujenzi wa Miundombinu hiyo hadi kukamilika kwa wakati.
Aidha Viongozi hao wa Dini pamoja na Wazee Maarufu wamemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa jitihadambalimbali anazofanya katika kuhakikisha kuwa anafufua Uchumi na Sekta mbalimbali zilizoathiriwa na Janga la UVIKO 19 huku wakiahidi kuwa mabalozi kuyatangaza mafanikio hayo kwa Wananchi.
Mashaka Nassor Kakulukulu,Sheikh wa Mkoa wa Katavi ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imefanikisha utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa ubora wa hali ya juu na kueleza kuwa jambo hilo ni kiashiria kuwa fedha iliyotolewa imetumika kikamilifu.
“Hakuna Ushahidi Mzuri kama ushahidi wa kujionea,tumekuja kujionea namna ambavyo miradi hii imetekelewa kwa fedha za Fedha za IMF na kwa kuwa tumejionea kila mtu anaona wazi kuwa kazi imefanyika kikamilifu, watoto wetu zamani walisoma katika vyumba ambavyo havikuwa vizuri lakini sasa hivi tunajionea vyumba vimekamilika kwa ubora wa ahali ya juu na watoto watasoma vizuri”alaisema Sheikh Kakulukulu.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Moravian Mpanda Mjini Ernest Simpanzye amesema ni vema wananchi wakatambua kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha kuwa inafufua sekta zilizoathiriwa na Janga la UVIKO ambapo licha ya Kumshukuru na kumpngeza Rais Samia amewataka Wananchi kumuuunga mkono katika mambo yote ya kimaendeleo anayolifanyia Taifa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe amempongeza Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Fedha nyingi kwa ajili ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba Nsimbo imeshuhudia mapinduzi makubwa kimaendeleo katika awamu hii ya sita.
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ilikamilisha Ujenzi wa Vyumba 87 vya Madarasa hadi kufikia 31 Desemba 2021 na kukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi vyumba hivyo 10 Januari 20211 ambapo kazi hiyo imekamilika kwa asilimia 100.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA.
Picha 1:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko(Mwenye Ushungi Mweusi) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Nsimbo mara baaada ya kuwasili Shule ya Sekondari Uruwira katika ziara yake akiambatana na Viongozi wa Dini na Wazee maarufu wa Mkoa wa Katavi.
Picha 2:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Wazee Maarufu pamoja na viongozi wa dini(Hawapo pichani)katika moja ya madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO 19 katika ziara yake Shule ya Sekondari Uruwira kukagua miradi hiyo akiambatana na Wazee maarufu na viongozi wa Dini.
Picha 3;Wazee Maarufu pamoja na Viogozi wa Dini wa Mkoa wa Katavi wakimsikiliza Mh.Mkuu wa Mkoa wa Katavi mara baada ya ukaguzi wa majengo ya UVIKO ndani ya moja kati ya vyumba vya madarasa ya UVIKO yaliyokamilika katika Shule ya Sekondari Uruwira.
Picha 4;Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe akitoa salamu za Shukrani kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi kukagua miradi ya UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Uruwira.
Picha 5;Sheikh wa Mkoa wa Katavi Mashaka Nassor Kakulukulu akizungumza kwa niaba ya Viongozi wa Dini mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa ya UVIKO 19 yaliyokamilika katika shule ya Sekondari Uruwira katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akiambatana nao kukagua miradi hiyo.
Picha 6;Mchungaji wa Kanisa la Moravian Mpanda Mjini Ernest Simpanzye akitoa salamu za shukrani wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya UVIKO 19.
Picha 7;Diwani wa Kata ya Uruwira Mh.Yusuph Mlela nae alipata wasaa wa kutoa salamu za Shukrani kwa Rais Samia mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh,Mwanamvua Mrindoko katika Ziara hiyo.
Picha 8;Muonekano wa Vyumba viwili vya Madarasa Lot 1 vilivyokamilika kwa Fedha za UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Uruwira.Shilingi Mil 80 zilielekezwa Uruwira kwa ajili ya Ujenzi.
Picha 9;Muonekano wa Vyumba viwili vya Madarasa Lot 2 vilivyokamilika kwa Fedha za UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Uruwira.Shilingi Mil 80 zilielekezwa Uruwira kwa ajili ya Ujenzi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa