Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Hoza Mrindoko(Katikati) akikabidhi Zawadi mbalimbali kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kasim Majaliwa kwa Uongozi wa Kituo cha Gethsemane kilichopo Kata ya Litapunga Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo 10 Novemba 2021.
Na:John Mganga-IO Nsimbo DC
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko amekabidhi zawadi mbalimbali kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kasim Majaliwa kwa kituo cha kulelea watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu cha Gethsemane kilichopo katika Kata ya Litapunga Halamashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Zawadi zilizokabidhiwa kwa Yatima na waishio katika Mazingira Magumu Gethsemane Nsimbo ni pamoja na Ngombe mmoja,Kilo 120 za Mchele, Lita 20 za Mafuta ya kupikia, Boksi mbili kubwa za Biskuti,pamoja na Pakti nane za Pipi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Zawadi hizo kwa Viongozi wa Kituo Hicho cha Gethsemane Mh.Mwanamvua amesema Mh.Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ametoa zawadi hizo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kufuatia kuguswa na kutambua uwepo wa watoto Yatima na waishio katika Mazingira magumu katika Kituo hicho.
Mh.Mwanamvua licha ya pongezi kwa Shirika la Upendo na Sadaka linalosimamia Yatima na Waishio katika Mazingira Magumu Gethsemane, amewataka Viongozi wa Shirika hilo kufanikisha maono mazuri waliyonayo ya Uanzishaji wa Kituo cha Kulea watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Magumu kwa kuhakikisha kuwa Sheria,Miongozo na Kanuni mbalimbali za uanzishaji na uendeshaji wa Vituo vya kulelea Yatima na waishio katika Mazingira magumu zinazingatiwa.
Amesisitiza kuwa Lengo la Serikali kuweka Sheria,Kanuni na Miongozo mbalimbali inayosimamia uanzishwaji na uendeshwaji wa vituo hivyo ni kuhakikisha kuwa Watoto wanaolelewa katika Vituo hivyo wanalelewa kwa kuzingatia Utaratibu.
Aidha Mh.Mwanamvua amesema ni muhimu Kituo hicho kuwajenga watoto katika misingi ya Maadili ya Kiroho kusudi watoto hao wakue katika Misingi ya kumjua Mwenyezi Mungu na kwamba endapo jambo hilo litatiliwa mkazo Taifa litakuwa na hazina ya Raia wenye Hofu ya Mungu jambo litakalopunguza na kuondoa kabisa changamoto ya mmomonyoko wa Maadili ya Taifa.
Katika Taarifa yake Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Kiongozi wa Mlezi ya watoto Kituoni hapo licha ya jitihada mbalimbali wanazochukua amezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa Mabweni pamoja na Changamoto ya Mawasiliano kituoni hapo .
Regina Marius, mmoja wa watoto waishio Kituoni hapo akitoa shukrani kwa niaba ya Watoto wenzake amemshukuru Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kusema kuwa daima watamkumbuka katika maombi kusudi Mwenyezi Mungu amjalie mafanikio katika Safari yake ya uongozi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Shirika hilo,Mwenyekiti wa Kamati ya Shirika hilo Sister Bernadetha Kihumbi amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kasim Majaliwa kwa msaadaa alioutoa Kituoni hapo na kuahidi kumuombea kwa Mungu ili kusudi azidishiwe pale alipopunguza kusaidia watoto wa Kituo hicho.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa