Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo wamesema kutokana na ziara yao ya kuongeza uwezo wa kuisimamia maswala ya kiutawala kwenye Halmashauri, kubuni vyanzo vya mapato na Kwenda kutembelea bandari ya Tanga kujifunza namna ya kuiendasha na usimamizi sasa wanaenda kuhakikisha Halmashauri inakuwa kinara katika Nyanja zote za ukuaji.
Kauli hizo wamezitoa baada ya kutembelea na kuona miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Chalinze miradi ya uchakataji ya kokoto za ujenzi, soko kubwa la machinga, hospitali ya Halmashauri hiyo na kituo cha matangazo ya radio wamesema wamejifunza na wanenda kuyatumia yote waliyoyapata.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Halawa malendeja amesema wameamua kufika kujifunza kwenye Halmashauri ya chalinze kutokana na Halmashauri hiyo kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato hivyo chaguo lao limegusa mahitaji ya wanansimbo.
Katika ziara hiyo ambayo Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe alikuwa miongoni mwa ziara hiyo amesema ziara hiyo imelenga kuwapatia mafunzo madiwani kwa lengo la kuona wenzao namna wanavyozisimamia Halmashauri Pamoja na namna ya kukusanya mapato.
Ziara ya madiwani hao lengo kubwa ni kujifunza namna ya utawala, ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa bandari ambapo wametembelea Halmashauri ya Chalinze na leo watahitimisha katika Mkoa wa Tanga kwa kutembelea bandari.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa