Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ulianza kutekelezwa rasmi Tarehe 1 Februari 2017 na ulitarajiwa kumalizika Tarehe 30 Julai 2018 ikiwa ni jumla ya Miezi 18.
Hata hivyo utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi huu uliathiriwa na Fedha za mradi kutowasilishwa kwa wakati hivyo kupelekea mradi kutokamilika kwa wakati uliopangwa.
Kwa sasa mradi huu unatarajiwa kumalizika Tarehe 17 Desemba 2021
Mradi huu unasimamiwa na Mjenzi Mshauri ambae ni Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MCB)
Aidha Mradi huu unajengwa na Kikosi cha Ujenzi(SUMA JKT)
Mradi huu mpaka kukamilika utagharimu Jumla ya Shilingi 3,145,719,168.00
Mjenzi Mshauri,Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MCB) atalipwa Jumla ya Shilingi 210,000,000.00
Mkandarasi kikosi cha Ujenzi(SUMA JKT)atalipwa jumla ya Tsh.2,935,719,168.00
Aidha Malipo ambayo yamefanyika mpaka sasa ni kama ifuatavyo;
Mpaka hivi sasa Mkandarasi amelipwa Jumla ya Tsh.1,330,895,760.72
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa