Pichani:Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Damas Ngassa(Katikati) akitoa maelekezo wakati wa zoezi la Upimaji wa mashamba katika Kijiji cha Kasisi kabla ya Wapima Wasaidizi na Wasimamizi kuingia katika mashamba na maeneo ya Wananchi kwa shughuli ya Upimaji.
Zoezi la Urasimishaji mashamba na makazi kwa ajili ya utoaji wa hatimiliki za Kimila Katika Kijiji cha Kasisi kinachotekeleza Mpango wa matumizi bora ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo limekamilika kwa mafanikio makubwa Afisa Ardhi Nsimbo Bw.Damas Ngassa ameeleza.
Idadi kubwa ya Wananchi katika Kjiji cha Kasisi wamejitokeza kurasimisha Maeneo ya makazi pamoja na Mashamba kufuatia Elimu na Hamasa iliyotolewa kwa makundi mbalimbali kuhusu faida za Urasimishaji Ardhi pamoja na umuhimu wa hatimiliki za Kimila ambapo zaidi ya hatimiliki za Kimila 3000 zinatarajiwa kuandaliwa na kutolewa bure kwa Wananchi wa Kijiji cha Kasisi waliojitokeza kurasimisha maeneo yao.
Zoezi hilo lililodumu kwa takribani siku 30 limehusisha Vitongoji Vinne vya Kijiji cha kasisi ambavyo ni Iseka,Kasisi,Iyogelo na Mabiti likifadhiliwa na Taasisi ya JGI(Jane Goodal Istitute)chini ya Mradi wa LCWT(Landscape Conservation in Wester Tanzania) ambapo Wananchi katika maeneo hayo wamepimiwa maeneo yao bure na mara baada ya taratibu za uhakiki na uandaaji kukamilika Wananchi hao watapatiwa Hatimiliki bure bila malipo yoyote.
Afisa Ardhi Nsimbo Bw.Damas Ngassa ameeleza kuwa zoezi la Urasimishaji maeneo ya makazi pamoja na mashamba katika Kijiji cha Kasisi limefanyika kwa kuwahusisha Wataalamu wa Ardhi kutoka Ofisi ya Ardhi Nsimbo, Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa pamoja na baadhi ya Wananchi ambao walitoka katika Kijiji cha Kasisi ambapo Taasisi ya JGI pia ilifadhili Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wananchi hao ili waweze kushiriki utekelezaji wa zoezi hilo kama Wapima Wasaidizi wakishirikiana na Wajumbe wa Kamati ya ardhi ya Kijiji kama Wahakiki kwa kutumia Teknolojia ya Vishkwambi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa